#MICHEZO: Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Yusuph Mwenda, amezindua bBodi mpya ya Klabu ya michezo ya TRA United, akieleza kuwa timu hiyo ni mkakati wa kiuchumi wa kuhamasisha ulipaji kodi wa hiari nchini.

Kupitia sekta ya michezo, TRA imelenga kuboresha taswira yake ya kujenga uelewa kwa jamii kuwa kodi ndiyo chanzo kikuu cha maendeleo, huku sekta binafsi ikitarajiwa kuchangia zaidi ya asilimia 70 ya rasilimali katika utekelezaji wa Dira ya Maendeleo ya 2050.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya TRA United Sports Club, Edmund Kawamara, ameahidi kusimamia klabu hiyo kwa nidhamu na uwajibikaji, ili kulinda rasilimali za umma na kuongeza mzunguko wa fedha katika sekta ya michezo.

Mwenda amesisitiza kuwa kuimarisha mifumo rafiki ya kodi na kupanua wigo wa walipa kodi kutapunguza utegemezi wa misaada ya nje na kuwezesha uwekezaji mkubwa katika miundombinu na huduma za jamii zinazochochea ukuaji wa uchumi wa taifa.

‎Powered by #MCHEZOSUPA


‎JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
‎-
‎Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

‎#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
‎#Follow @itvtz @radioonetanzania
‎@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *