#HABARI: Serikali imefanikiwa kuokoa kiasi cha Shilingi bilioni sita, kupitia mfumo wa manunuzi ya pamoja ya saruji na vifaa vya ujenzi kwa ajili ya ujenzi wa vyuo vya VETA katika wilaya 64 nchini na mkoa wa Songwe.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda, amebainisha kuwa mkakati huo pamoja na msamaha wa kodi umesaidia kupunguza gharama za ujenzi, huku serikali ikiwa imetenga Shilingi bilioni 100 kwa ajili ya kuimarisha miundombinu hiyo ya elimu ya ufundi.

Akizungumza wakati wa uwekaji jiwe la msingi la Chuo cha VETA wilayani Same, Prof. Mkenda amesisitiza kuwa ujenzi wa vyuo hivyo ni utekelezaji wa maono ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuwaandaa vijana kwa ajira na maendeleo ya kiuchumi.

‎Powered by #MCHEZOSUPA


‎JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
‎-
‎Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

‎#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
‎#Follow @itvtz @radioonetanzania
‎@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *