#HABARI: Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Bashiru Ally Kakurwa, amesema kuwa kiapo alichokula alipoteuliwa kushika wadhifa huo kinamtaka kusimamia kwa dhati maslahi ya wafugaji, ikiwa ni pamoja na kuwaondoa katika umasikini na kukomesha vitendo vya utapeli vinavyowaathiri.
Waziri Bashiru ametoa kauli hiyo Jijini Tanga, wakati wa kikao maalum cha kutathmini hali ya utendaji wa kiwanda cha kusindika maziwa cha Tanga Fresh na kujadili mikakati ya kukinusuru.
Amesisitiza kuwa kiapo chake kinamlazimisha kusimamia sekta ya mifugo kwa misingi ya tija, ufanisi na uendeshaji wa kibiashara, huku akilenga kuhakikisha manufaa yanawafikia wafugaji na Taifa kwa ujumla.
Akizungumzia maazimio ya kikao hicho, Waziri Bashiru alielekeza kufanyika kwa ukaguzi maalum wa kiuchunguzi kwa kipindi cha miezi miwili kuanzia Machi 1, 2026. Ukaguzi huo unalenga kubaini mwenendo wa matumizi ya fedha za kiwanda hicho na kuweka msingi wa maboresho ya kiutendaji na kiusimamizi.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania