#HABARI: Serikali ya Mkoa wa Shinyanga imeutaka uongozi wa mgodi wa dhahabu wa Kikundi cha Mchapakazi Nyandolwa (W) Shinyanga uliokuwa umepata ajali Agosti 11,2025 na kusababisha watu 25 kufukiwa chini ya ardhi kuendelea kufanya ukarabati wa maduara 22 ya uchimbaji ili yakidhi vigezo vya kuruhusiwa kuendelea na uzalishaji baada ya mgodi kufungwa, huku maduara 44 kati ya maduara 66 yaliyokaguliwa yakionekana kuwa ni hatarishi na kufungiwa yasiendelee kufanya shughuli zozote za uzalishaji wa madini.
Kauli hiyo ameitoa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mboni Mhita wakati akitembelea mgodi huo na kueleza kuwa Timu ya wataalamu wa Serikali iliyofika Nyandolwa kufanya uchunguzi wa kina wa ajali hiyo iliyotokea Agosti 11, 2025 ambayo iliua watu 22, baada ya ukaguzi huo ilishauri hatua mbalimbali zichukuliwe iliwemo maduara hatarishi kufungiwa ili kuhakikisha usalama wa wachimbaji wadogo.
Katika hatua nyingine Serikali ya Mkoa wa Shinyanga imetoa kibali kwa mgodi wa HHH and Partners ulioko jirani na mgodi huo wa wachapakazi ambao nao ulipata madhara katika tukio hilo la kuporomoka kwa maduara ya mgodi wa wachapakazi kuendelea na shughuli za uchimbaji baada ya Serikali kujiridhisha huku Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mboni Mhita akiwataka wamiliki wa leseni za uchimbaji kufuata taratibu na miongozo ya usalama hatua kwa hatua ili kuzuia maafa kama hayo yasijirudie.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania
Powered by #MCHEZOSUPA