Tanzania sasa ina uwezo wa kuzalisha jumla ya megawati 4,400 za umeme, huku matumizi ya sasa yakiwa megawati 2,071, hali inayotoa ziada ya umeme inayoweza kuimarisha sekta ya viwanda na shughuli za uzalishaji.
Taarifa hiyo imetolewa leo Februari 20, 2026, baada ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini kukagua miradi mikubwa ya umeme mkoani Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa kamati hiyo, Subira Mgalu amesema uwepo wa ziada ya umeme umepunguza kwa kiasi kikubwa changamoto za kukatika kwa umeme na kuondoa kabisa mgao, jambo linalochochea uendelevu wa biashara na uwekezaji.
Mgalu pia amesisitiza umuhimu wa TANESCO kuendelea kuimarisha miundombinu ya usambazaji, ikiwemo njia za kutoka Bwawa la Julius Nyerere hadi Chalinze, Kinyerezi hadi Mkuranga, kuhakikisha umeme unawafikia watumiaji wa viwanda na wajasiriamali wadogo.
Serikali inalenga kufikia uzalishaji wa megawati 8,000 ifikapo 2030 ili kukidhi mahitaji yanayoongezeka. Mpango huo unalenga pia kuongeza upatikanaji wa umeme kwa takribani wananchi milioni 1.7 kila mwaka, huku sekta binafsi ikipatiwa uhakika wa nguvu ya umeme kwa ajili ya uwekezaji na ukuaji wa kiuchumi.
#AzamTVUpdates
Mhariri | John Mbalamwezi

(Feed generated with FetchRSS)