Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Heart Team Africa Foundation iliyo chini ya Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Mussa Azan Zungu amesema Serikali inachangia asilimia 70 ya gharama za matibabu ya moyo kwa watoto ikiwa ni sehemu ya juhudi za kupambana na tatizo hilo nchini.
Akizungumza jijini Dar es Salaam baada ya kikao cha bodi ya taasisi hiyo kilicholenga kupanga mikakati ya upatikanaji wa fedha, Zungu amesema takribani watoto 10,000 huzaliwa kila mwaka wakiwa na matatizo ya moyo, hivyo kuwataka wadau mbalimbali kujitokeza kuchangia ili kusaidia matibabu hayo.
#AzamTVUpdates
✍Estabela malisa
Mhariri | John Mbalamwezi
(Feed generated with FetchRSS)