#HABARI: Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini imeeleza kuridhishwa na kuimarika kwa hali ya nishati nchini, ambapo sasa uwezo wa uzalishaji umefikia megawati 4,400 dhidi ya mahitaji ya megawati 2,071.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Subira Mgalu, ametoa pongezi hizo baada ya kukagua vituo vya Kinyerezi I na II pamoja na kituo cha kusafirisha umeme kwenda Zanzibar cha Ras Kilomoni, akibainisha kuwa kukatika kwa umeme kumepungua na hakuna mgao kwa sasa.
Aidha, Serikali kupitia Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu, Mhe. Innocent Luoga, imesisitiza dhamira ya kufikia maono ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuzalisha megawati 8,000 ifikapo mwaka 2030.
Kamati imeshauri TANESCO kuelekeza nguvu zaidi katika ujenzi wa miundombinu ya usafirishaji ili nishati hiyo iwafikie walaji wa mwisho, hususan katika maeneo ya viwanda na migodi, huku lengo likiwa ni kuunganishia umeme takribani wananchi milioni 1.7 kila mwaka.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.