Wakazi wa Walaya ya Hai wameendelea kunufaika na uwepo wa Hifadhi ya Taifa Kilimanjaro (KINAPA) hususani kupitia mfuko wa ujirani mwema.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), Wilayani Hai, alipokuwa akijibu hoja za baadhi ya wananchi waliudhuria Mkutano wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mwigulu Lameki Nchemba (Mb) na wananchi wa Wilaya hiyo, Mkoani Kilimanjaro.
Dkt. Kijaji amebainisha kuwa, kwa nyakati tofauti KINAPA imekuwa ikiwezesha miradi ya ujenzi wa shule 9, nyumba ya mwalimu, kumalizia maabara, na ununuzi wa samani.
“Thamani ya miradi hii ni shilingi milioni 346,794,195”. Alisema Dkt. Kijaji
Aidha, aliwataka wananchi hao, kuendelea kuitunza Hifadhi hiyo, kama sehemu ya kuunga mkono jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan za kuinua sekta ya uhifadhi na Utalii, kwa kuwa mapato yanayopatikana kutoka kwenye Hifadhi hiyo na zinginezo, zinachangia siyo tu uchumi wa mtu mmoja mmoja bali kwenye huduma mbalimbali za jamii nchini.
Naye Mwalimu Mkuu wa Shule ya Wasichana Kilimanjaro Bi. Mariana Denis Msangi, akiwasilisha taarifa ya Shule yake kwa Waziri Mkuu Mh. Dkt. Mwigulu Nchemba, ameipongeza Wakala wa Usimamizi wa Misitu Tanzania (TFS), kwa mchango mkubwa wa miche ya miti 12000 na mbao za kutengenezea samani za Shule na madawati.
#StarTvUpdate
(Feed generated with FetchRSS)