
Mwanaume
mwenye silaha ameuawa kwa kupigwa risasi baada ya kuingia katika eneo la makazi
ya Rais wa Marekani Donald Trump huko Mar-a-Lago, Florida, imesema Idara ya
Usalama wa rais.
Mwanaume
huyo alikuwa amebeba bunduki na kopo la mafuta aliposimamishwa kabla ya kupigwa
risasi na maafisa wa Secret Service na polisi, imesema Idara hiyo.
Tukio hilo
lilitokea Jumapili asubuhi, wakati rais alipokuwa Washington DC.
Mshukiwa
ametajwa kama Austin T Martin kutoka Cameron, North Carolina, kulingana na CBS.
Familia yake
huko North Carolina iliripoti kupotea kwake mapema Jumapili asubuhi, Ofisi ya Polisi
ya Kaunti ya Moore imesema katika taarifa kwa BBC.
Ofisi hiyo
imesema haina historia yoyote ya uhalifu inayomhusu Martin.
Mwanaume
huyo alipigwa risasi baada ya kukataa amri, amesema mkuu wa polisi wa kaunti ya
Palm Beach, Ric Bradshaw.
“Maneno
pekee tuliyomwambia yalikuwa ‘acha vitu hivyo’ ikimaanisha kopo na bunduki,”
Bradshaw aliuambia mkutano na waandishi wa habari.
“Aliweka
chini kopo la gesi, akainua bunduki yake hadi mahali pa kufyatua risasi,”
alisema.
Maafisa
walimpiga risasi.
Aliongeza
kuwa maafisa hao walikuwa wamevaa kamera za mwili na hakuna maafisa waliojeruhiwa.
Usalama huko
Mar-a-Lago ni mkali sana, ukiwa na uzio wa nje wa polisi wa Palm Beach na ule
wa ndani unaosimamiwa na Idara ya Usalama wa rais.
Trump
amekuwa shabaha na majaribio kadhaa ya mauaji.
Julai 2024,
Trump alipigwa risasi sikioni alipokuwa amesimama mbele ya umati wa watu huko
Butler, Pennsylvania.