Chad imevifunga vivuko kadhaa vya mpaka wake na Sudan siku ya Jumapili, pamoja na sehemu muhimu ya Adre na pia Darfur Magharibi, ili kuzuia makundi yenye silaha ya Sudan kuvuka kuingia katika eneo

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Maafisa wa usalama pamoja na wafanyabiashara katika eneo hilo la mpaka kati ya Chad na Sudan wanasema Hatua hiyo inakuja wakati huu kukishuhudia mapigano kati ya jeshi la Sudan na washirika wake dhidi ya Kikosi cha RSF katika eneo la Tine la Darfur Kaskazini na maeneo kaskazini mwa mji mkuu wa jimbo la Darfur Magharibi, El Geneina.

Mwishoni mwa juma lililopita Vyombo vya habari vya Chad viliripoti kwamba wapiganaji wa RSF walishambulia kambi ya jeshi la Chad katika mji wa Tine, na kusababisha majeruhi kadhaa na kuharibu magari ya kijeshi.

Hata hivyo Mamlaka ya Chad haijatoa taarifa yoyote kuhusu mzozo huo ulioripotiwa, na sasa Jeshi la Chad limeimarisha usalama kwenye êneo hilo, huku wanajeshi wengi wakipelekwa kando ya mpaka na Darfur Magharibi , wakati vikosi vya ziada vikipelekwa katika kivuko cha Tine huko Darfur Kaskazini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *