Waziri Mkuu wa Greenland Jens-Frederik Nielsen ameikataa ofa ya Rais wa Marekani Donald Trump ya kutuma meli ya hospitali katika eneo hilo la Denmark linalojiendeshea mambo yake, ambalo Trump amekuwa akilifuatilia kwa muda mrefu ili kulinyakua.

Siku ya Jumamosi, Trump alisema atatuma “boti kubwa ya hospitali” kwenye kisiwa cha Aktiki ili kuhudumia kile alichokiita “watu wengi ambao ni wagonjwa, na hawahudumiwi.”

Siku ya Jumapili, Nielsen alimjibu Trump katika andiko aliloweka kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook akisema: “itakuwa ni hapana asante inayotoka hapa.”

Waziri mkuu wa Greenland ameendelea kueleza katika jibu lake kwa Trump: “Wazo la Rais Trump la kutuma meli ya hospitali ya Marekani hapa Greenland limefahamika vizuri. Lakini sisi tuna mfumo wa huduma ya afya ya umma ambapo matibabu yanatolewa kwa raia bila ya malipo”, kinyume na ulivyo mfumo wa Marekani.

Hata hivyo, Nielsen alisisitiza kwamba, mazungumzo yatahitaji kupewa heshima maamuzi ya ndani ya Greenland.

Naye Waziri wa Ulinzi wa Denmark Troels Lund Poulsen amesema, kisiwa hicho hakihitaji msaada usio wa kuomba kutoka kwa Trump.

“Jamii ya Greenland inapokea huduma ya afya inayohitajia,” ameeleza waziri huyo alipozungumza na chombo cha habari cha Denmark DR siku ya Jumapili, akibainisha kuwa raia hupatiwa msaada wa matibabu kisiwani humo au nchini Denmark…/

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *