Venezuela imewaslisha ombi rasmi kwa Umoja wa Mataifa ikitaka kuachiwa huru mara moja Rais wa nchi hiyo Nicolas Maduro, kufuatia kutekwa nyara na wanajeshi wa Marekani katika operesheni ya mapema mwezi Januari mwaka huu ambayo Caracas imeitaja kuwa ‘kinyume cha sheria’.

Yvan Gil Pinto Waziri wa Mambo ya Nje wa Venezuela ametaka kuachiwa huru haraka iwezekanavyo Rais Maduro na mkewe Cilia Flores ambao wanashikiliwa New York wakisubiri kufunguliwa mashtaka. Waziri wa Mambo ya Nje wa Venezuela ameeleza haya jana katika mkutano wa Baraza la Haki za Binadamu la UN mjini Geneva Uswisi. 

Maduro amekana kuhusika na magendo ya madawa ya kulevya na akijitaja kuwa ‘mateka wa vita.”

Maduro alitekwa nyara katika ikulu ya rais huko Caracas mji mkuu wa Venezuela na kuhamishiwa katika gereza moja huko New York akisubiri kesi yake akituhumiwa kuongoza genge la mihadarati na magendo ya silaha. 

Yvan Gil Pinto amelaani mashambulizi ya kijeshi ya Marekani dhidi ya Venezuela yaliyouawa watu zaidi ya 100 nchini humo.

“Licha ya “tofauti kubwa ya kimlingano kwa upande wa  kiteknolojia na kijeshi” kati ya Venezuela na “Marekani inayomiliki nguvu ya nyuklia ,Caracas imechagua “kufungua njia ya kidiplomasia ili kuzipatia ufumbuzi  hitilafu zilizopo kati ya nchi mbili.”

Kwa upande wake Rais Donald Trump wa Marekani amekuwa akitamka wazi kwamba anadhibiti kikamilifu sekta ya mafuta ya Venezuela kufuatia wanajeshi wa Marekani kumteka nyara rais wa nchi hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *