Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Sayyid Abbas Araghchi amesema kwamba mafanikio ya mazungumzo yatategemea upande wa pili kuyachukuliwa kwa uzito na kujiepusha na tabia na misimamo inayokinzana.

Araghchi alisema hayo jana alipokutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Oman, Badr Al-Busaidi. mjini Geneva,  kabla ya kufanyika duru ya tatu ya mazungumzo ya nyuklia yasiyo ya moja kwa moja kati ya Jamhuri ya Kiislamu na Marekani, yanayotazamiwa kufanyika katika jiji la hilo la Uswisi leo Alkhamisi.

Wakati wa mkutano huo, hoja na mambo ya kuzingatia ya Iran kuhusu suala la nyuklia na kuondolewa kwa vikwazo haramu na vya upande mmoja vya Marekani dhidi ya nchi hiyo vilielezwa.

Wakati huo huo, Araghchi amesema, muelekeo wa Iran kuhusiana na mazungumzo hautaathiri mamlaka ya kujitawala ya taifa.

Kwa upande wake, Al-Busaidi alisifu uthabiti wa Jamhuri ya Kiislamu katika kufuata mbinu ya kidiplomasia katika suala la nyuklia, akisisitiza utayari wa Oman kuendelea na ofisi zake nzuri na kutoa msaada wowote katika njia hii.

Alielezea matumaini kwamba, kwa uzito wa pande zote mbili kutoka kwa pande zinazohusika katika mazungumzo, mazungumzo hayo yatasababisha matokeo ya kuridhisha pande zote mbili.

Huku Marekani ikizidisha mvutano katika eneo la Asia Magharibi ili kutishia Iran kwa kupeleka manowari za kijeshi karibu na Ghuba ya Uajemi, Jamhuri ya Kiislamu inasisitiza kwamba, haitakubali kulazimishwa kusitisha kikamilifu urutubishaji wa urani na kueleza kwamba, makombora ya Iran hayana nafasi katika mazungumzo hayo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *