Ofisi ya pamoja ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa, mwishoni mwa juma lililopita imetoa tahadhari kuhusu kukithiri kwa vitendo vya utumwa wa ngono na kuongezeka kwa idadi ya watoto wanaozaliwa kutokana na ubakaji.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Ofisi hiyo imesema ubakaji umekuwa ukitumika kama silaha ya vita hali ambayo inaharibu hatma ya watoto wanaozaliwa kutokana na ukatili huo.

Kwa mujibu wa takwimu za mwaka jana, matukio 887 ya udhalilishaji wa kingono yaliripotiwa  huku kukiwa na waathiriwa 1534 , ambao  854 walikuwa ni wanawake na 672 wakiwa wasichana.

Aidha asilimia 80 ya vitendo hivyo viliripotiwa mashariki mwa nchi katika mikoa ya Kivu Kaskazini na Kivu ya Kusini.

Wapiganaji Wazalendo wanaosaidiana na serikali ya Congo katika vita dhidi ya waasi wa M23.
Wapiganaji Wazalendo wanaosaidiana na serikali ya Congo katika vita dhidi ya waasi wa M23. AP – Moses Sawasawa

Ripoti inasema makundi ya waasi yalichangia asilimia 75 ya  dhulma hizo ,waasi wa M23 wakiongoza wakifuatiwa na wapiganaji wazalendo ,CODECO , Mai Mai  na FDLR, huku jeshi la serikali FARDC na polisi wakitajwa kuhusika kwenye udhalimu huo.

Umoja wa Mataifa sasa unataka pande husika kwenye mgogoro wa nchi hiyo kusitisha mapigano na kutoa nafasi ya misaada ya kibinadamu kuwafikia wahanga wa vita pamoja na jumuiya ya kimataifa kuongeza ufadhili wa kifedha.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *