
Nchini Senegal, chama tawala, PASTEF, kimeamua kuchukuwa msimamo dhidi ya muungano wa “Diomaye rais”. Wakati mzozo ukiongezeka kati ya Rais Bassirou Diomaye Faye na Waziri wake Mkuu, Ousmane Sonko, maafisa wengi wa Pastef wamechukua msimamo—katika kipindi cha saa 24 zilizopita—wakimtetea kiongozi wa chama chao, Ousmane Sonko.
Imechapishwa:
Dakika 2 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Msimamo huu unaelekezwa dhidi ya muungano wa “Diomaye rais”, ambao ulifanya mkutano wake mkuu wa kwanza siku ya Jumamosi, Machi 7, na unajipanga kuwa nguvu mbadala ya PASTEF katika uchaguzi ujao.
Msimamo huu unaelekezwa dhidi ya muungano wa “Diomaye rais”, ambao ulifanya mkutano wake mkuu wa kwanza siku ya Jumamosi, Machi 7, na unajipanga kuwa nguvu mbadala ya PASTEF katika uchaguzi ujao.
Ousmane Sonko, “mlinzi wa mapinduzi,” ni ujumbe ambao mechapishwa kwenye ukurasa wa Facebook wa msemaji wa serikali Marie Rose Faye. Vivyo hivyo kwa Waziri wa Utumishi wa Umma, Olivier Boucal. Katika saa za hivi karibuni, maafisa wa chama cha PASTEF wamekuwa wakichagua pande kupitia mitandao ya kijamii. Kwa wengi, wanasema kuunda nguvu ya kisiasa kama mbadala wa PASTEF ni usaliti wa rais Bassirou Diomaye Faye kwa chama kilichomleta madarakani.
“Bassirou Diomaye Faye anawezaje ghafla kujitenga na wale waliounda jukwaa hilo wakati alichaguliwa kwa ajili ya sera za chama cha siasa? Haina maana. Anasaliti sera za PASTEF. Anateka nyara uhamasishaji mkubwa na maarufu wa raia wa Senegal,” anasema Guy Marius Sagna, mbunge wa PASTEF.
Na vipi kuhusu deni kubwa la umma?
Upinzani pia umechanganyikiwa, kwa deni kubwa la umma na matatizo ya kiuchumi yanayokuja ambayo yanatokana na vita nchini Iran, na kusikitishwa na mgawanyiko huu kati ya Mkuu wa Nchi na Waziri Mkuu wake. “Badala ya kuhamasisha nguvu zote kuwa na mwamko wa kitaifa na kushughulikia matatizo,” amesema Thierno Alassane Sall, mbunge huru, “Sonko na Diomaye wanaongeza mgawanyiko huo. Sasa ni matatizo badala ya suluhisho.”
Tangu Jumamosi, Ousmane Sonko hajatoa tamko lolote kuhusu mkutano huu wa muungano wa “Diomaye rais”, ambao unatakiwa kutumika kujiandaa kwa “uchaguzi ujao,” kama ilivyoainishwa katika katiba yake. Hata hivyo, mnamo Machi 1, kiongozi huyo wa PASTEF aliwasihi wafuasi wake kutozingatia sana muungano huu, ambao, kulingana naye, hauwezi kushindana na chama cha PASTEF.
