Trump asema oparesheni za kijeshi nchini Iran zitamalizika karibuniTrump asema oparesheni za kijeshi nchini Iran zitamalizika karibuni

Rais wa Marekani, Donald Trump, amesema operesheni za jeshi la nchi yake nchini Iran zitamalizika karibuni, akitoa hakikisho kwa masoko ya dunia ambayo yametetereka kutokana na mzozo unaoendelea mashariki ya kati.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Kauli ya Trump, anaitoa wakati ambapo jeshi lenye nguvu nchini Iran likidai lenyewe ndilo litakaloamua vita iishe lini, wakati huu pia likiapa kuwa tiifu kwa kiongozi mpya wa juu wa kidini, Mojtaba Khamenei.

Masoko ya dunia yalikuwa yameporomoka kutokana na vita vya Mashariki ya kati, bei za mafuta zikionekana kupanda Jumatatu ya wiki hii.

Mwanamke akiwa na picha ya kiongozi mpya wa juu wa Iran Ayatollah Mojtaba Khamenei jijini Tehran, Jumatatu 9 Machi 2026.
Mwanamke akiwa na picha ya kiongozi mpya wa juu wa Iran Ayatollah Mojtaba Khamenei jijini Tehran, Jumatatu 9 Machi 2026. AFP – ATTA KENARE

Tehran chini ya uongozi wa kiongozi wake mpya Mojtaba Khamenei, imeendelea kurusha makombora kuelekea majirani zake katika nchi za Ghuba, ikiaashiria kwamba mfereji wa Hormuz huenda ukaendelea kufungwa.

Licha ya Rais Trump kudai kwamba vita hivyo vinakaribia kumalizika, jeshi la mapinduzi la Iran limetupilia mbali kauli yake kuhusu vita hivyo likisema kwamba ndilo litakaloamua ni lini vita vitamalizika.

Tangazo la Trump limejiri wakati huu wanajeshi wa Iran wakiripotiwa kuanzisha mashambulio mapya ya makombora na droni katika nchi za Saudi Arabia, Bahrain, Qatar,UAE na Israel.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *