
Tangu kuanza kwa vita kati ya Marekani na Israel dhidi ya Iran, nchi zinazotawaliwa na wanajeshi barani Afrika zimebaki bila kuegemea upande wowote. Waziri Mkuu wa Mpito wa Mali alitoa salamu zake za rambirambi baada ya kifo cha Ali Khamenei, lakini bila kuidhinisha au kulaani upande wowote.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Hii ni kwa sababu ESA imeanzisha tena uhusiano na Washington katika miezi ya hivi karibuni, haswa kupitia juhudi mpya katika miradi ya usalama na maendeleo. Hata hivyo, wafuasi wa serikali za kijeshi wamejiunga na utawala wa Iranna wanaongeza machapisho yao kwenye mitandao ya kijamii, ambayo Taasisi ya Timbuktu imeyachambua kwa makini.
“Wanaharakati wa mitandao walio karibu na serikali za kijeshi zilizoko madarakani Sahel wanajaribu kubadilisha, hata kwa mfano, ndege zisizo na rubani za Iran kuwa somo la uhuru, wakifurahia mapungufu ya Marekani na ndoto zao kuzielekeza Global South ambayo inakataa kutii, ingawa serikali za kijeshi za ESA (Mali-Niger-Burkina Faso) tayari zinajadiliana nyuma ya pazia kuhusu kurudi kwa Marekani kwa Sahel. Ni hali ya kutofautiana kabisa,” anaelezea Bakary Sambe, kiongozi wa Taasisi ya Timbuktu Institute huko Dakar.
“Iran inaonekana mara moja kama mfano wa upinzani na uhuru, ikionyesha matarajio ya nchi za ESA na hivyo kuiunganisha Iran na vita dhidi ya Magharibi, hata dhidi ya Ufaransa, huko Sahel,” anaongeza.
Waangalizi wengi na wadau wa kisiasa, ikiwa ni pamoja na nchini Marekani na Ulaya, wameibua suala la mashambulizi haya kuwa kinyume cha sheria, yanayofanywa kwa amri ya Marekani na Israel nje ya mfumo wowote wa kisheria wa kimataifa.
Kuhusu wanaharakati wa mitandao wanaounga mkono nchi za Sahel, hakuna hawazungumzi lolote kuhusu maelfu ya vifo vya nchini Iran vinavyotokana na utawala wa mbaya wa nchi hiyo. Bakary Sambe anabainisha hili: “Kinyume chake, kuna aina za mshikamano na Iran, ambazo zinachukuliwa kama ishara ya upinzani ambazo zinapaswa pia kututia moyo hapa Sahel.”