Kiongozi mpya wa juu wa  Iran Mojtaba Khamenei  yupo salama licha ya taarifa za kujeruhiwa wakati wa mashambulizi ya Marekani na Israeli, amethibitisha Yousef Pezeshkian, mtoto wa Rais wa Iran.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Yousef ambaye ambaye pia ni mshauri wa serikali ya Iran, amethibitisha hili kupitia ukurasa wake wa Telegram.

“Nilisikia ripoti kwamba bwana Mojtaba Khamenei alikuwa amejeruhiwa. Nimewauliza baadhi ya watu wa karibu. Wameniarifu kwamba yupo salama.” alisema Yousef Pezeshkian.

Televisheni inayomilikiwa na serikali ya Iran awali ilikuwa imemtangaza Khamenei kama “shujaa wa vita vya mwezi wa Ramadan” bila ya kutaja jeraha alilolipata.

Посольство Ірану в Москві. 2 березня 2026
Посольство Ірану в Москві. 2 березня 2026 © AP

Mojtaba Khamenei ni mtoto wa pili wa kiongozi wa muda wa Iran Ayatollah Ali Khamenei, ambaye aliuuawa katika mashambulio ya Israeli na Marekani Februari 28, mauaji yake yakisababisha sintofahamu ya uongozi kwenye taifa hilo.

Mojtaba mwenye umri wa miaka 56, tangu kuchukua uongozi wa Iran wiki iliopita hajatoa taarifa yoyote wala kulihutubia taifa.

Gazeti la The New York Times likiwanukuu baadhi ya maofisa wa katika serikali ya Iran, limesema  Khamenei “alipata majeraha, ikiwemo kwenye miguu yake na kwamba alikuwa apelekwa katika eneo salama, na kwamba yupo salama”.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *