
Vita vimeendelea kwenye eneo la Mashariki ya Kati, ambapo Marekani na Israeli zimeendelea kuishambulia Iran na Lebanon, huku Iran nayo ikirusha makombora katika nchi za Ghuba, katika mzozo unaoendelea kusababisha maafa na uharibu mkubwa.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Wakati vita vikiendelea, meli tatu za mizigo zimeshambuliwa na kuharibiwa na makombora katika eneo la Bahari ya Hormuz siku ya Jumatano.
Meli hizo zilikuwa na watu 23, na walionekana wakiokolewa, huku meli yao ikifuka moshi.
Awali jeshi la Marekani, lilisema limeharibu meli 16 za Iran zinazoaminiwa kuwa na silaha baharini.
Iran nayo imeendeleza mashambulio yake kwa kurusha makombora nchini Saudi Arabia, nchi ya Falme za Kiarabu, Qatar na Kuwait, huku ikisema Israel na Marekani zimeshambulia maeneo zaidi ya elfu 10 yanayokaliwa na raia wa kawaida.
Aidha, Iran inasema watu zaidi ya 1,300 wameuawa tangu kuanza kwa vita hivyo siku 11 zilizopita.
Israeli nayo imeendeleza mashambulio ya angaa nchini Lebanon, na kulenga maakazi ya watu katikati mwa jiji la Beirut na maeneo mengine ya nchi hiyo.