Waziri wa Ulinzi wa Israeli Israel Katz ametangaza mnamo Machi 11 kwamba mashambulizi yaliyoanzishwa kwa pamoja na Israel na Marekani dhidi ya Iran mnamo Februari 28 yataendelea “bila kikomo.” Asubuhi ya leo, Israel imetangaza kuwa imeshambulia katikati na vitongoji vya kusini mwa Beirut. Wizara ya Afya ya Lebanon inaripoti kwamba watu wasiopungua 570 wamefariki tangu mwanzoni mwa mwezi Machi.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Kituo cha katikati mwa mji mkuu wa Lebanon kimeshambuliwa mapema Jumatano asubuhi. Vitongoji vya kusini mwa Beirut, ngome ya Hezbollah inayounga mkono Iran, vililengwa na mashambulizi mengi ya Israel siku ya Jumanne na Jumatano, huku Lebanon ikiwa imerekodi zaidi ya watu 760,000 waliokimbia makazi yao na vifo 570 tangu mwanzoni mwa mwezi Machi.
Jeshi la Israel pia limetangaza kuwa limezindua mfululizo mpya wa mashambulizi dhidi ya Tehran, baada ya kulenga eneo la chini ya ardhi linalomilikiwa na Kikosi cha Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) katika mji mkuu wa Iran usiku wa kuamkia Jumatano.
Angalau meli tatu zilishambuliwa leo Jumatano karibu na Mlango-Bahari wa Hormuz, ambao umekuwa kitovu kikuu cha kimkakati cha vita katika Mashariki ya Kati, na kusababisha hatari ya kuvurugika kwa uchumi wa dunia.
Iran “haiogopi” “vitisho tupu” vya Donald Trump, amesema Ali Larijani, mkuu wa Baraza Kuu la Usalama wa Kitaifa la Iran, akimjibu rais wa Marekani. Spika wa bunge la Iran, kwa upande wake, alionya kwamba nchi yake italipiza kisasi “jicho kwa jicho, jino kwa jino” kwa shambulio lolote dhidi ya miundombinu yake. Siku ya Jumanne, Iran ilirusha makombora mengine kuelekea Israel na malengo ya Marekani katika Mashariki ya Kati.