
Katika ripoti iliyochapishwa mnamo Februari 27, Tume ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini ilishutumu vikosi vya Uganda kwa kuingilia kati pamoja na jeshi la Sudan Kusini katika operesheni zilizowaua raia. Katika taarifa iliyotolewa siku ya Jumanne jioni, Machi 10, jeshi la Uganda lilikana shutuma hizi.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Na mwandishi wetu jijini Nairobi, Gaëlle Laleix
“Haijawahi kutokea katika historia yake ya miaka 45 kwamba jeshi la Uganda liliwalenga raia, ndiyo maana ni maarufu sana popote lilipofanya kazi,” Wizara ya Ulinzi ya Uganda iliandika katika taarifa.
Kulingana na Wizara, matokeo ya operesheni ya Uganda nchini Sudan Kusini ni ya kushangaza. Haikuzuia tu mapigano huko Juba, mji mkuu, lakini “pia ilizuia mashambulizi ya wanamgambo wa White Army dhidi ya raia,” wanamgambo wa kabila la Nuer, la pili kwa ukubwa nchini.
Ilikuwa mwezi Machi 2025 ambapo jeshi la Uganda liliingilia kati kulinda Juba, kwa ombi la mamlaka ya Sudan Kuini, ambayo wakati huo ilikuwa chini ya shinikizo kutoka kwa makundi mbalimbali ya waasi. Lakini Tume ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa inabaini kwamba vikosi vya Uganda pia vilishiriki kikamilifu katika mapigano katika maeneo yanayopinga serikali.
Walipiga mabomu “maeneo yaliyojaa raia wa Nuer.” Umoja wa Mataifa unalaani vifo vingi, majeraha makubwa ya kuungua, na uharibifu wa nyumba.
Jeshi la Uganda tayari limeingilia kati mara mbili nchini Sudan Kusini: mnamo mwaka 2013 mwanzoni mwa vita vya wenyewe kwa wenyewe, kisha mnamo mwaka 2016, kila wakati pamoja na Rais Salva Kiir.