
Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa anatarajiwa katika mji mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati leo Alhamisi, Machi 12. Ingawa mkutano na Rais Faustin-Archange Touadéra unatarajiwa, kutoka kwa mtazamo wa Paris, ziara hii pia ni fursa ya kutathmini maendeleo yaliyopatikana katika kurejesha uhusiano na Jamhuri ya Afrika ya Kati tangu marais wa nchi hizo mbili walipokubaliana mapendekezo mnamo mwezi Aprili 2024.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Hili halijawahi kutokea tangu mwezi Novemba 2018. Kwa mara ya kwanza katika zaidi ya miaka saba, Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa anazuru Bangui, mji mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR), leo Alhamisi, Machi 12.
Jean-Noël Barrot anakuja kuunga mkono mipango kadhaa: mradi wa Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD) kupambana na mafuriko, nyumba ya Mosuca ya shirika la Waathirika wa Unyanyasaji wa Kijinsia, mchezo wa kuigiza unaopangwa kwa Tamasha lijalo la Avignon, kihifadhi biashara cha Bangui Hub, na maabara mpya ya marejeleo ya utafiti wa polio itakayozinduliwa katika Taasisi ya Pasteur.
Katika upande wa kisiasa, mkutano na Rais Faustin-Archange Touadéra pia unatarajiwa, kufuatia wiki yake nchini Urusi, ambayo ilijumuisha ziara ya “kibinafsi” huko Saint Petersburg na mazungumzo huko Moscow ambapo Vladimir Putin alimhimiza “kuratibu misimamo yao katika jukwaa la kimataifa,” ingawa bado haijulikani wazi ikiwa mpango wa Urusi wa kutaka Africa Corps kuchukuwa nafasi ya Wagner umeendelea.
Kwa mtazamo wa Paris, ziara hii pia, na zaidi ya yote, ni fursa ya kuona maendeleo yaliyopatikana katika kurejesha uhusiano kati ya nchi hizo mbili na athari “chanya” zinazoonekana za mapendekezo ya mwezi Aprili 2024. Hati hii ambayi ilikubaliwa na marais wa Ufaransa na Jamhuri ya Afrika ya Kati, imelenga “kufufua” uhusiano wa pande mbili kati ya Ufaransa na Jamhuri ya Afrika ya Kati, pamoja na kuihusisha tena Paris nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Ingawa mamlaka ya Ufaransa imeanza tena misaada ya kifedha na ushirikiano na Jamhuri ya Afrika ya Kati tangu wakati huo, pia imekubali kuchaguliwa tena kwa Rais Touadéra mwishoni mwa mwezi Desemba, chini ya masharti yanayopingwa na upinzani. Kwa upande mwingine, kampeni za kupinga Ufaransa zimepungua kwa kiasi kikubwa huko Bangui.