s

Chanzo cha picha, Reuters

Wananchi wa Jamhuri ya Congo (Brazzaville) wanapiga
kura leo Jumapili katika uchaguzi wa rais unaotarajiwa kwa kiasi kikubwa kuongeza
muda wa utawala wa kiongozi wa muda mrefu Denis Sassou Nguesso, mwenye umri wa
miaka 82, kwa kipindi kingine cha miaka mitano.

Uchaguzi huo unafanyika huku upinzani ukiwa
dhaifu na kukiwa na hali ya kutokuwa na mashaka makubwa kuhusu matokeo.

Viongozi wawili maarufu wa upinzani bado
wanashikiliwa gerezani, huku wengine wakiwa uhamishoni nje ya nchi. Baadhi ya
vyama vya upinzani vimesusia uchaguzi huo vikisema mchakato wake hauna
uaminifu.

Zaidi ya wapiga kura milioni 3.2 wamesajiliwa
kushiriki katika uchaguzi huo, ingawa wachambuzi na makundi ya kiraia
wanatarajia idadi ya wapiga kura kujitokeza kwa uchache ikilinganishwa na karibu
asilimia 68 iliyorekodiwa mwaka 2021, wakati Sassou Nguesso aliposhinda kwa
kupata asilimia 88.4 ya kura.

Kiongozi huyo alichukua madaraka mwaka 1979
katika taifa hilo la Afrika ya Kati linalozalisha mafuta, na ametawala karibu
bila kukatizwa tangu wakati huo, isipokuwa kwa kipindi cha miaka mitano katika
miaka ya 1990.

Katika uchaguzi huu anakabiliwa na wagombea
sita ambao hawajulikani sana, na hakuna anayeonekana kuwa mpinzani mkubwa, huku
taasisi nyingi za uchaguzi zikidaiwa kutawaliwa na watu wanaoegemea chama
tawala cha Congolese Labour Party.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *