#HABARI: Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt. James Mataragio, ameiagiza Mamlaka ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA) kuimarisha shughuli za utafutaji wa mafuta na gesi asilia ambazo zimepungua kwa kiasi kikubwa.
Dkt. Mataragio amebainisha kuwa idadi ya mikataba ya uzalishaji na ugawanaji mapato (PSA) imeporomoka kutoka 26 hadi 11, hali inayohitaji mikakati madhubuti ya kuvutia wawekezaji wapya ili kuhakikisha usalama wa nishati nchini.
Dkt. Mataragio amesisitiza kuwa kupungua kwa kasi ya utafutaji ni hatari kwa mustakabali wa upatikanaji wa gesi asilia, kwani hatua hiyo ndiyo msingi wa ugunduzi wa rasilimali mpya.
Ili kurekebisha hali hiyo, Wizara imejipanga kuboresha mazingira wezeshi ya uwekezaji yatakayochochea kampuni za kimataifa kurejea na kutekeleza majukumu yao ya utafutaji kikamilifu katika vitalu vilivyopo nchini.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa PURA, Mhandisi Charles Sangweni, amesema wameanza kutekeleza mikakati mipya ikiwemo kuingia mikataba na makampuni ya kijiofizikia kwa ajili ya kukusanya takwimu za petroli.
Hatua hiyo inalenga kuimarisha utafiti katika maeneo ya bahari kuu na nchi kavu ili kutoa picha halisi ya rasilimali zilizopo, jambo litakalosaidia kuongeza thamani ya vitalu vya Tanzania katika soko la Kimataifa.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
-
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.