#HABARI: Wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani wamepongeza hatua ya Serikali kutenga zaidi ya hekari 20,000 katika maeneo matatu kwa ajili ya uanzishaji wa kongani za viwanda.
Hatua hiyo imekuja siku chache baada ya ITV Digital kuripoti kero ya utiririshaji wa majitaka kutoka viwandani, ambapo sasa wakazi hao wakiongozwa na Bw. Abduhashimu Msati na Bw. Waziri Mrema, wanaamini kuwa maeneo hayo mapya yatatoa suluhu ya kudumu ya mazingira na kelele zilizokuwa zikiwaathiri katika makazi yao.
Mkuu wa Idara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji wa Halmashauri hiyo, Bwana Idrisa Jukulu, amebainisha kuwa mkakati huo unalenga kuhakikisha maeneo hayo yanakuwa wezeshi na rafiki kwa uwekezaji wa kisasa.
Kwa kutenga maeneo hayo maalum, halmashauri inakusudia kuimarisha usimamizi wa viwanda na miundombinu ya majitaka, jambo litakalochochea ukuaji wa uchumi wa wilaya bila kuathiri afya na ustawi wa jamii inayozunguka.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
-
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.