#HABARI: Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Mhe. Subira Mgalu, amesema Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) inaendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya kusambaza umeme ili kuhakikisha wananchi wanaoishi pembezoni mwa miji na vijijini wanapata huduma hiyo muhimu kwa maendeleo ya kijamii na kiuchumi.
Akizungumzia mafanikio ya Miradi ya kusambaza umeme Machi 15, 2026 katika Kitongoji cha Elimu Kijiji cha Mshinde mkoani Geita, Mhe. Subira Magalu alisema kuwa Miradi inayotekelezwa inalenga kupanua wigo wa huduma ya umeme katika vitongoji 15 kwa kila jimbo la uchaguzi HEP 2(A) pamoja na Mradi mkubwa wa kusambaza umeme kwenye vitongoji 9,009 Tanzania nzima Geita ikiwemo.
Aidha, Mwenyekiti huyo wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini ameigaza Kampuni ya CCC Beijing Industrial & Commercial Co. Ltd ambayo inatekeleza Miradi mingi mkoani Geita kuhakikisha hadi kufikia Machi 28, 2026 inakamilisha miradi ambapo kwa sasa utekelezaji wake ulikuwa umefikia asilimia 80.
Kwa upande wake Naibu Waziri, Wizara ya Nishati, Mhe. Salome Makamba amewapongeza Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini kwa kuendelea kuisimamia vyema Sekta ya Nishati pamoja na ukaribu wao katika kufuatilia Miradi ya kusambaza nishati ya umeme hadi kwenye vitongoji.
Powered by #MCHEZOSUPA:
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.