#HABARI: Serikali imetoa pongezi na zawadi kwa wakaguzi na Askari waliopo chini ya Vyombo vya Usalama, vilivyopo chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ambao walijitoa na kufanya vizuri zaidi, akiwepo Askari wa Jeshi la Magereza, Festo Bupilipili ambaye siku za hivi karibuni ilisambaa picha kwenye mitandao ya kijamii akionekana kuwafunika kwa koti lake wanafunzi ili wasilowe na mvua iliyokua ikinyesha mkoani Morogoro, tukio ambalo lilivuta hisia za watanzania wengi.
Pongezi na zawadi hizo zimetolewa jijini Dodoma na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi kando ya Ufunguzi wa Mafunzo ya Kuwajengea Uwezo Maafisa Mapokezi wa Wafungwa ikiwa ni Utekelezaji wa maelekezo ya Rais wa Tanzania, Dkt.Samia Suluhu Hassan, aliyoyatoa kupitia Tume ya Haki Jinai ambapo alielekeza Maboresho ya Vyombo vya Haki Jinai ikiwemo Uandaaji na Utekelezaji wa Programu za Urekebishaji.
Waziri Katambi amesema, wapo askari wengi wanaofanya matendo ya utu nchi nzima ikiwa ni mafunzo na maelekezo wanayofundishwa wakiwa mafunzoni huku wengine pia wakisukumwa na utu kufanya matendo hayo mema kwa jamii, huku akiweka wazi waliopongezwa leo ni uwakilishi wa askari wengi nchi nzima wanaofanya kazi zao kwa juhudi na bidii.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania