Rais wa Belarus Alexander Lukashenko, aliwasilisha pendekezo hilo katika ikulu ya Urusi wakati wa mkutano na Rais Vladimir Putin aliyeonekana kuunga mkono hadharani wazo hilo.

Lukashenko amesema kiwanda hicho kinaweza kutumika ikiwa kitahitajika kusambaza nishati katika maeneo yanayodhibitiwa na Urusi ya Kherson, Zaporizhzhia, Luhansk, na Donetsk.

Kiwanda cha Belarus cha Astravets kilifadhiliwa na mkopo wa Urusi

Belarus ilifungua kiwanda chake cha kwanza cha nguvu za nyuklia cha Astravets  mnamo Novemba 2020. Kiwanda hicho kilijengwa na shirika la serikali ya Urusi la nishati ya atomiki, Rosatom, kwa mkopo wa dola bilioni 10 uliotolewa na Moscow.

Hata hivyo katika mkutano wa leo, Putin hakufafanua ikiwa Urusi itafadhili ujenzi wa kiwanda hicho kipya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *