katika Kijiji Cha Mahiga Kata ya Mwang’halanga Wilaya ya Kwimba Mkoani Mwanza ambapo mgogoro baina ya viongozi wa sungusungu ulisababisha mgawanyika Mkubwa Kwa viongozi wa jeshi Hilo la jadi na kufanya serikali ya Kijiji kufungwa Kwa siku kadhaa huku wananchi wakihangaika kupata huduma za serikali ya Kijiji

Baadhi ya wakazi wa Kijiji hicho akiwemo Mashaka Nderema na Masalu Makoye wamesema mgogoro mvutano baina viongozi wa sungusungu umekwamisha shughuli za maendeleo hivyo kutatuliwa kwake utasaidia kuweka juhudi za pamoja katika kuchochea maendeleo

Mkuu wa wilaya ya Kwimba Mkoani Mwanza Ng’wilabuzu Ludigija amesema Jeshi la jadi la Sungusungu limekuwa msaada Mkubwa katika kukabiliana na vitendo vya kihalifu kwenye vijiji na Kata kwenye maeneo mbalimbali hivyo ameelekeza kiongozi wa Sungusungu Kanda hiyo kusimamia uchaguzi ili kupata viongozi wapya watakaotekeleza majukumu yao Kwa weledi.

Aidha Ludigija ameitaka serikali ya Kijiji hicho kulisimamia kikamilifu jeshi la jadi la Sungusungu ili litekeleze majukumu yake Kwa ufanisi na kuhakikisha vitendo vya kihalifu vinakoma katika Kijiji Cha Mahiga Kwa mustakabar Bora wa maendeleo ya Kijiji hicho.

Ifahamike kuwa taratibu za kupata viongozi wapya wa sungusungu katika Kijiji Cha Mahiga Kata ya Mwang’halanga zimekamilika na tayari viongozi wapya wamepatiiana ambao wameahidi kuchapata kazi maradufu.

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *