
Waziri wa zamani nchini Kenya, Raphael Tuju alikamatwa hapo jana Jumatatu saa chache baada ya kuonekana tena hadharani kufuatia ripoti za kutoweka kwake.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Mkuu wa idara ya upelelezi nchini Kenya Mohammed Amin amemtuhumu Tuju kwa kupanga njama ya utekaji wake ilhali alikuwa amejificha nyumbani kwake.
Familia yake ilikuwa imedai ametekwa kabla yake kujitokeza na kukiri alienda mafichoni siku ya Jumamosi baada ya kuhisi kuwa kuna watu waliokuwa wakimfuata.
Tuju ameendelea kugonga vichwa vya habari nchini Kenya, kutokana na kwamba alishindwa kulipa mkopo kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika Mashariki, na sasa benki hiyo inataka kuchukua mali yake, Tuju akituhumu baadhi ya watu mashuhuri serikalini kwa kuhusika kwenye mzozo huo.