Iran imepokea mpango wa mapendekezo 15 kutoka kwa Marekani kuhusu namna ya kumaliza vita vinavyoendelea Mashariki ya Kati, huku Tehran ikisema Marekani inashauriana peke yake kuhusu kumaliza vita.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Ripoti zinasema kuwa, Iran imepokea mapendekezo hayo kutoka kwa Pakistan ambayo, imesema iko tayari kusaidia kufanikisha mazungumzo hayo.

Hata hivyo, mpango huo haujawekwa wazi, lakini ripoti za ndani zinaeleza kuwa baadhi ya mambo yanayopendekezwa ni kuwa, Iran iachane kabisa na mradi wa Nyuklia, ili vikwazo vyote vya kiuchumi ilivyowekewa viondolewe.

Waziri mmoja wa Israeli amesema  mapendekezo hayo yanaonekana maridadi kwenye makaratasi, lakini hana uhakika iwapo Iran itaikubali.

Katika hatua nyingine, jeshi la Iran limepuuzilia mbali mapendekezo ya Marekani na kuahidi kuendelea kupigana.

Licha ya jitihada hizi za kuwepo kwa mazungumzo, wanajeshi wa Marekani na Israli wameendelea kuishambulia Iran, ambayo pia imeendelea kurusha makombora yake nchini Israeli.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *