Ripoti ya Umoja wa mataifa inasema familia nyingi zilizokimbia makazi yao kwenye majimbo matatu ya Kordofan nchini Sudan hazijapokea msaada wowote wa kibinadamu katika miezi mitatu iliyopita.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Katika ripoti hiyo UN Women imesema Kanda ya Greater Kordofan kwa sasa inahifadhi zaidi ya watu milioni moja waliokimbia makazi yao, karibu nusu yao wakiwa wanawake na wasichana.

Idadi ya watu waliokimbia makazi yao katika eneo hilo imeongezeka kwa asilimia kumi na tano, na wengi wao hawakupokea msaada wowote huku Wale waliopokea msaada wakiuelezea kuwa hautoshi kwa mahitaji yao ya msingi.

Matokeo hayo yalitokana na utafiti wa mashirika 43 yanayoongozwa na wanawake na majadiliano na viongozi wa jamii za wanawake wanaotoa msaada wa kibinadamu wakiwa mstari wa mbele katika eneo lote.

Ripoti hiyo ilionya kuhusu ukosefu wa usalama wa chakula, ikibainisha kuwa zaidi ya nusu ya familia zilizokimbia makazi yao huko Kordofan Kusini zilikuwa zimekaa mchana na usiku mzima bila chakula katika mwezi mmoja kabla ya utafiti huo.

Upatikanaji wa huduma ya afya pia umepungua, huku ripoti za wanawake wakipata mimba wakiwa njiani huku wakikimbia migogoro na vifo vya watoto wachanga vinavyosababishwa na uhaba mkubwa wa chakula.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *