Chanzo cha picha, Reuters
Waziri wa
Mambo ya Nje wa Iran Abbas Araghchi amesema katika mahojiano ya televisheni ya
taifa ya Iran kwamba kwa “siku kadhaa” Marekani “imeanza kutuma
ujumbe mbalimbali kupitia wapatanishi tofauti”.
Lakini amesema
ukweli kwamba jumbe hizi “ziliwasilishwa kupitia nchi rafiki”, na
kwamba Iran ilikuwa ikijibu kwa kusema “misimamo yao na kutoa
maonyo”, “sio mazungumzo wala majadiliano, wala chochote cha aina
hiyo”.
Araghchi pia
amesema kwamba sera ya Iran kwa sasa ni kuendelea “kujitetea”, na “hawana nia ya kujadiliana kwa sasa”.
Anaongeza
kwamba, “Hii ni vita vya Israeli na watu wa eneo hilo na watu wa Marekani
wanalipa gharama yake.”
Kilichofanyika
hivi karibuni kuhusu mazungumzo kati ya Marekani na Iran?
Kilichotokea
kufikia sasa:
- Waziri wa Habari wa Ikulu ya Marekani Karoline Leavitt amesema siku ya Jumatano, Rais Trump amekuwa akishiriki katika “mazungumzo yenye tija” na Iran kwa siku tatu zilizopita.
- Pia alisema hatua hiyo ilikuwa “imefanyika kwa haraka” na utawala wa Iran ulikuwa unatafuta “njia ya kutokea”
- Ujumbe huo ni tofauti kabisa na sauti ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Abbas Araghchi, ambaye baadaye alisema kwamba Iran ” haina nia ya kufanya majadiliano kwa sasa ”
- Alisema ujumbe “umewasilishwa kupitia nchi rafiki”, lakini mabadilishano haya “si mazungumzo wala majadiliano, wala kitu chochote cha aina hiyo”
- Bila kukata tamaa, Trump anasisitiza kwamba Iran “inajadiliana”, akisema ” wanaogopa kusema hivyo kwa sababu wanafikiri watauawa na watu wao wenyewe”. Aliongeza: “Pia wanaogopa watauawa na sisi”
- Pia kumekuwa na ripoti zinazokinzana kuhusu mapendekezo ya kukomesha vita. Siku ya Jumatano, kulikuwa na ripoti kwamba Iran ilikuwa imepokea mpango wa vipengele 15 kutoka Marekani kwa ajili ya kufikia makubaliano ya kusitisha mapigano.
- Kwa upande wake, “afisa mwandamizi wa usalama wa kisiasa” wa Iran alinukuliwa na mtangazaji wa serikali Press TV akisema walikuwa na masharti matano ya kukomesha vita, ikiwa ni pamoja na malipo ya “fidia ya vita” na kumaliza vita katika nyanja zote.
- Wakati huo huo, mapigano yanaendelea – moshi ulionekana ukitoka kwenye kituo cha umeme cha Israeli baada ya kuripotiwa kwa shambulio la kombora la Iran, huku mifumo ya ulinzi wa anga ya Iran ikisikika mjini Tehran.
Soma zaidi: