Jeshi la Israel, leo Alhamisi, Machi 26, limesema kwamba limekuwa likijibu mashambulizi ya makombora ya Iran yaliyorushwa kuelekea Israel. Falme za Kiarabu pia zinakabiliwa na mashambulizi ya ndege zisizo na rubani na makombora yanayotoka Iran.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Watu wawili wamejeruhiwa kidogo katika mji wa Kiarabu katikati mwa Israel kufuatia kombora moja au zaidi lililorushwa kutoka Iran, kulingana na Idara za dharura za Israel. Magen David Adom, sawa na shirika la Msalaba Mwekundu la Israel, limeripoti kwamba watu wawili wenye umri wa miaka hamsini “wamejeruhiwa na mlipuko huo” huko Kafr Qassem (katikati mwa Israel), na kuongeza kwamba waathiriwa, ambao walipata majeraha madogo, wametibiwa katika eneo la tukio.

Jeshi la Israel linasema linajibu mashambulizi ya makombora ya Iran

Jeshi la Israel limesema leo Alhamisi kwamba limekuwa likijibu mashambulizi ya makombora ya Iran yaliyorushwa kuelekea Israel, huku ving’ora vya mashambulizi ya anga vikilia katikati mwa nchi, sehemu za Jerusalem, na Ukingo wa Magharibi unaokaliwa. “Mifumo ya ulinzi wa anga iko katika hatua za kuzuia tishio hilo,” jeshi limesema katika taarifa, zaidi ya saa 14 baada ya shambulio lililoripotiwa hapo awali.

Falme za Kiarabu zinasema zinajibu mashambulizi ya ndege zisizo na rubani na makombora kutoka Iran

Falme za Kiarabu zimesema leo Alhamisi kuwa zinajibu mashambulizi ya ndege zisizo na rubani na makombora kutoka Iran. “Ulinzi wa anga unajibu vitisho vya makombora na ndege zisizo na rubani kutoka Iran,” Wizara ya Ulinzi ya UAE imesema kwenye mtandao wa kijamii wa X.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *