Tamasha maarufu la kukuza utamaduni na utalii nchini litafanyika jijini Mwanza Aprili 19, ikiwa ni mara ya pili
Mwaka jana Machi 8 lilifanyika jijini Mwanza na kuutangaza utamaduni wa makabila mbalimbali nchini, huku likiwavutia zaidi ya watazamaji 5000
Tamasha hiloLilifanyika katika viwanja vya Furahisha na kuweka historia ya kuwa tamasha pekee lililoyatangaza makabila mbalimbali nchini, huku likiwavutia wadau wengi
Waandaaji, Cheza Kidansi Entertainment wanasema maandalizi yanaendelea vizuri ili mwaka huu tamasha liweke historia ya kuwavutia watu zaidi ya 10,000 na kuutangaza utamaduni mzuri wa kitanzania, makabila mbalimbali pamoja na kuutangaza mkoa wa Mwanza na vivutio kibao
Matukio makubwa yatachukua nafasi yake siku hiyo kwa maboresho makubwa zaidi ikiwemo mbio fupi za wakimbiaji zaidi ya 1,000, ngoma za makabila mbalimbali, michezo ya asili zikiwemo sarakasi, bao, mdako, vyakula kibao vya asili vitakavyopikwa na kuliwa uwanjani, maonesho ya mavazi, utani wa makabila, burudani za muziki wa asili na hotuba fupi za wadau
Hakuna kiingilio, wananchi wote wanakaribishwa kuja kuburudika, kuelimika, kupata taarifa mpya za utalii, utamaduni, kula vyakula vya asili, kushiriki mbio na kuondoa msongo wa mawazo, kikubwa wavae mavazi ya asili
Waandaaji wamewaomba wadhamini wengi wadhamini tamasha hilo la siku 2 ili wapewe nafasi kubwa ya kujitangaza, kuuza bidhaa, huduma, kuwafikia wateja wao, kuongea nao na kuwapa elimu ya shughuli zao
Tamasha hilo kwa kiwango kikubwa litautangaza mkoa wa Mwanza pamoja na fursa nyingi zilizopo mkoani humo na Kanda ya ziwa ikiwemo utalii wa utamaduni
Chief Hangaya Utamaduni Festival litafanyika kwa siku 2 na kuwapa wadau na wajasiriamali kuuza, kujitangaza na kutengeneza faida kubwa zaidi
Litafanyika tarehe 19 na 20 Aprili 2026 kuanzia saa 12 asubuhi katika viwanja vya Furahisha jijini Mwanza
#StarTvUpdate

(Feed generated with FetchRSS)