#HABARI: Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), imetoa msaada wa mashine mbili za kisasa kwa ajili ya kutoa joto kwa Watoto Njiti katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Amana ambapo msaada huo unalenga kuokoa maisha ya watoto wanaozaliwa kabla ya wakati kwa kuwapatia huduma muhimu ya joto, ambayo ni ya msingi katika hatua za awali za uhai wao.
Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Crispin Chalamila, amesema hatua hiyo ni mwendelezo wa taasisi hiyo kurejesha kwa jamii kupitia michango ya watumishi wake.
Kwa upande wake, Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Amana, Dkt. Jumanne Ihoyelo, amesema mashine hizo zitapunguza changamoto ya upatikanaji wa vifaa tiba na kuongeza ufanisi katika kuwahudumia Watoto Njiti.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.
(Feed generated with FetchRSS)