
Wananchi katika nchi kadhaa za Afrika wamefanya maandamano wakipinga vita na mashambulizi ya Marekani na Israel dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Watu wa Ivory Coast, Cameroon na nchi nyingine kadhaa za Magharibi mwa Afrika wamefanya mikutano na maandamano makubwa ya kueleza mshikamano wao kamili na Iran na kulaani vikali uhalifu wa kijeshi unaofanywa na Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya nchi hiyo.
Raia wa Ivory Coast katika jiji la Kouroukoro wametangaza uungaji mkono wao mkubwa kwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa kutoa kaulimbiu kama vile “Mauti kwa Marekani” na “Mauti kwa Israel,” wakilaani vitendo vya uchokozi vya Rais wa Marekani Donald Trump na Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu dhidi ya Iran.
Washiriki katika maandamano hayo ambao wameonekana wakibeba picha za Kiongozi Mkuu wa Iran, Sayyid Mojtaba Ali Khamenei na mtangulizi wake Imam Khamenei aliyeuawa shahidi katika hujuma ya Marekani na Israel, wamesisitiza utiifu wao kwa kiongozi wa sasa wa Mapinduzi ya Kiislamu.
Huku wakitoa kaulimbiu kama vile “Labbaik ya Khamenei” na “Labbaik ya Iran,” washiriki wamesisitiza uhusiano wa kindugu kati ya nchi hizo na Jamhri ya Kiislamu na kutilia mkazo haja ya kuimarishwa umoja katika Umma wa Kiislamu dhidi ya sera za tawala za Washington na Tel Aviv.
Maandamno kama hayo pia yamefanyika katika miji kadhaa ya Ulaya na huko Marekani ambako washiriki wametangaza waziwazi upinzani wao dhidi ya vita vya kikatili vya Donald Trump na mshirika wake, nduli Ntanyahu wa Israel.