Mamlaka nchini DR Congo imetangaza siku ya leo Jumtano kuwa sikukuu ya kitaifa kusherehekea hatua ya timu ya taifa ya Leopards kufuzu kombe la dunia kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 52.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Leopards ilifuzu kombe la dunia Jumanne usiku baada ya kupata ushindi wa bao moja bila ya jibu dhidi ya Jamaica.

Taifa hilo la Afrika ya kati limeshiriki tu kombe la dunia mara moja mwaka wa 1974 wakati lilikuwa bado linajulikana kama Zaire.

Mchezaji wa zamani wa Manchester United Tuanzebe ndiye aliyeifungia DRC bao la kipekee katika daikika ya 100 ya mchezo.

Mashambiki wa Leopards wamesherekea hatua ya timu yao kufuzu kombe la dunia katika Miji mbalimbali haswa jijini Kinshasa.

Mechi ya kwanza ya DR Congo kwenye kombe la dunia itakuwa dhidi ya Ureno ya Christiano Ronaldo katika Mji wa Houston nchini Marekani Juni 17.

Watacheza pia dhidi ya Colombia na Uzbekistan katika hatua ya makundi. DR Congo ni nchi ya 10 ya Afrika kufuzu kombe la dunia la mwaka huu litakaloandaliwa katika nchi za Marekani, Mexico na Canada.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *