Chanzo cha picha, Reuters
Marekani,
Iran na kundi la wapatanishi wa kikanda wanajadili masharti ya uwezekano wa
kusitisha mapigano kwa siku 45 ambayo yanaweza kusababisha kukomeshwa kwa vita
kabisa, Axios iliripoti siku ya Jumapili, ikinukuu vyanzo vinne vya Marekani,
Israel na kikanda vyenye ufahamu wa mazungumzo hayo.
Reuters
haikuweza kuthibitisha ripoti hiyo mara moja. Ikulu ya White House na Idara ya
Mambo ya Nje ya Marekani hazikujibu mara moja maombi ya Reuters ya kutoa maoni.
Wapatanishi
wanajadili masharti ya makubaliano ya awamu mbili, ripoti hiyo ilisema,
ikiongeza kuwa awamu ya kwanza itakuwa usitishaji mapigano wa siku 45 ambapo
mwisho wa vita utajadiliwa.
Awamu ya
pili itakuwa makubaliano ya kukomesha vita, ripoti hiyo ilisema.
Ripoti hiyo
iliongeza kuwa kusitisha mapigano kunaweza kuongezwa muda ikiwa muda wa ziada
utahitajika kwa mazungumzo.
Rais wa
Marekani Donald Trump aliambia Wall Street Journal siku ya Jumapili kwamba
tarehe yake ya mwisho kwa Iran kufungua Mlango-Bahari wa Hormuz la sivyo
itakabiliwa na mashambulizi dhidi ya miundombinu muhimu Jumanne
jioni.
Soma zaidi: