#HABARI: Mbunge wa Jimbo la Kawe Mhe, Geofrey Timoth, ameshiriki katika uzinduzi wa ujenzi wa Kituo cha Polisi Tegeta, akisisitiza umuhimu wa kuimarisha usalama kwa wakazi wa eneo hilo na maeneo jirani.
Katika hafla hiyo iliyofanyika leo Jumatatu Aprili 6, 2026 jimboni kawe jijini Dar es Salaam, Mbunge huyo alieleza kuwa ujenzi wa kituo hicho ni hatua muhimu katika kusogeza huduma za kiusalama karibu na wananchi, sambamba na kupunguza vitendo vya uhalifu vinavyoweza kujitokeza kutokana na kukua kwa makazi na shughuli za kiuchumi.
Akiwa katika tukio hilo, Mbunge Timoth alipiga simu kwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud, ambapo walijadiliana kuhusu umuhimu wa kukamilisha ujenzi huo kwa wakati pamoja na kuimarisha miundombinu ya vyombo vya usalama nchini.
Mbunge huyo pia aliahidi kuendelea kushirikiana na Serikali na wadau mbalimbali kuhakikisha kituo hicho kinakamilika na kuanza kutoa huduma kwa ufanisi.
Kwa upande wao, wananchi wa Tegeta wameeleza matumaini yao kuwa uwepo wa kituo hicho utasaidia kuimarisha hali ya usalama na kuleta utulivu zaidi katika eneo hilo.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania
(Feed generated with FetchRSS)