Christopher Okello amekiri kuwachoma visu watoto wanne hadi kufa katika shule ya awali ya Ggaba iliyoko jijini Kampala nchini Uganda, akidai kuwa alifanya hivyo kama kafara ili kupata utajiri.

Waendesha Mashtaka wamesema mshtakiwa, Christopher Okello, mwenye umri wa miaka 39 ambaye ana uraia wa Uganda na Marekani, amefikishwa mahakamani na kusomewa mashtaka rasmi dhidi yake.

Aprili 2,2025, mshtakiwa huyo alifanikiwa kuingia katika shule hiyo baada ya kujifanya kuwa mzazi wa mtoto na kuwashambulia watoto kwa kisu, kisha kuwaua wanne kati yao.

#AzamTVUpdates
Mhariri | John Mbalamwezi

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *