Ujumbe Maalum wa Viongozi wa ACT Wazalendo umekutana na Mjumbe Maalum wa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola Lazarus Chakwera ambaye pia ni Rais Mstaafu wa Malawi.
Ujumbe huo ulioongozwa na Kiongozi wa Chama hicho Dorothy Semu, uliwajumuisha pia Makamu Mwenyekiti Zanzibar Ismail Jussa, Makamu Mwenyekiti Bara Isihaka Mchinjita na Katibu wa Mambo ya Nje Mwanaisha Mndeme.
Viongozi hao wamekabidhi kwa Chakwera Uchambuzi wa Chama hicho kuhusu Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025, Mauaji yaliyotokana na Vurugu za Oktoba 29, 2025 na Msimamo wa ACT Wazalendo Juu ya Mwelekeo wa Siasa Nchini.
#StarTvUpdate

(Feed generated with FetchRSS)