Chama cha Democratic Alliance nchini Afrika Kusini (DA), chama cha pili kwa ukubwa nchini humo, kimemchagua kiongozi mpya siku ya Jumapili, Machi 12, 2026, kufuatia uamuzi wa kiongozi anayeondoka, Waziri wa Kilimo John Steenhuisen, wa kutotaka kuwania tena.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu huko Johannesburg, Claire Bargelès

Geordin Hill-Lewis hatimaye alichaguliwa, licha ya kukabiliana na mpinzani mmoja tu, Sibusiso Dyonase ambaye hajulikani sana. Kabla ya kuchaguliwa kwake kama meya wa Cape Town mnamo mwaka 2021, alihudumu kama mbunge na kushikilia nyadhifa mbalimbali ndani ya chama.

Jina lake lilikubaliwa wajumbe wa chama, na kwa hivyo haikushangaza kwamba Geordin Hill-Lewis, akiwa na umri wa miaka 39, alichukua uongozi wa Chama cha Democratic Alliance (DA). Chama hicho kimemchagua tena kiongozi kijana, akifuata nyayo za mtangulizi wake, mwenye mawazo ya kisiasa ya kiliberali na azma ya kuifanya DA ivutie zaidi ya wapiga kura wake wa jadi wazungu na rangi mchanganyiko.

Geordin Hill-Lewis anataka kuendelea kuthibitisha kwamba chama chake kina uwezo wa kutawala, akikusudia kudumisha wadhifa wake kama meya wa Cape Town mbali na uchaguzi wa serikali mitaa uliopangwa kufanyika mwezi Februari mwakani. Hatarajiwi kuchukua wadhifa wa uwaziri katika serikali ya muungano ya kitaifa inayodhibitiwa na ANC, ili kudumisha uwezo wa kukosoa chama cha Cyril Ramaphosa.

Bado anahitaji kupata umaarufu nje ya ngome yake ya Cape Town, lakini tayari ana malengo yake katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2029: “Lengo letu lazima liwe kuongoza serikali ya kitaifa,” alitangaza baada ya mkutano mkuu wa chama.

Hatimaye, kwa wale ambao wangeikosoa DA kwa kupendelea tena mzungu, chama kinaangazia timu nyingine ya uongozi, yenye utofauti zaidi kuliko hapo awali, haswa na uchaguzi usiotarajiwa wa meya wa zamani wa Pretoria, Solly Msimanga, kwenye nafasi ya naibu kiongozi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *