Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Tanga ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), ikiongozwa na Mwenyekiti wake Rajabu Abdallah, imeanza ziara ya kukagua miradi ya ujenzi wa nyumba za watumishi katika mkoa huo, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuboresha mazingira ya kazi kwa watendaji wa serikali na chama
Ziara hiyo inayofanyika katika wilaya zote za Mkoa wa Tanga inalenga kufuatilia maendeleo ya utekelezaji wa miradi hiyo muhimu, huku mwenyekiti huyo akitarajiwa kutembelea wilaya zote za Mkoa wa Tanga na mpaka Sasa ametembelea Wilaya za Pangani, Tanga Jiji, Muheza na Korogwe.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo Wilayani Korogwe, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga Rajabu Abdallah amesema chama hicho kinaendelea kusimamia kwa karibu utekelezaji wa miradi ya maendeleo, ambapo katika nyumba 36 zitajengwa katika Wilaya zote, huku nyumba nyingine zikiwa zimeanza Ujenzi tayari.
Aidha, amesema kuwa ujenzi wa nyumba hizo ni sehemu ya ahadi aliyoitoa wakati wa kampeni za kuwania nafasi ya Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga, ambapo aliahidi kuhakikisha kila wilaya inakuwa na nyumba za watumishi na watendaji wa chama
Kwa sasa, ujenzi wa nyumba hizo unaendelea kwa kasi katika wilaya mbalimbali, hatua inayotafsiriwa kuwa chachu ya kuboresha utendaji kazi na huduma kwa wananchi katika Mkoa wa Tanga
(Feed generated with FetchRSS)