Donald Trump amemkosoa vikali Papa Leo XIV kwenye mitandao ya kijamii baada ya kiongozi wa kwanza wa Marekani wa Kanisa Katoliki Duniani kulaani tishio la rais wa Marekani dhidi ya Iran.

Katika chapisho refu kwenye mtandao wake wa kijamii wa Truth Social, rais huyo wa Marekani aliandi Papa “ni mbaya kwa Sera ya Kigeni”.

“Simtaki Papa ambaye anadhani ni sawa kwa Iran kuwa na Silaha ya Nyuklia,” Trump alisema.

Akiorodhesha malalamiko mengine dhidi ya Papa, Trump aliandika kwamba Papa ”hana nguvu kushughulikia uhalifu na silaha za nyuklia”.

Maoni ya Trump dhidi ya kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki, ambaye – ingawa anajulikana kwa kukisia matamshi yake – ameibuka kama mkosoaji mkubwa wa vita vya Marekani na Israel dhidi ya Iran.

Papa Leo alisema tishio la Bw Trump la “ataiangamiza Iran” isipofikia makubaliano ya kumaliza vita ”halikubaliki”.

Papa pia aliongeza kusema: “Kuna suala la sheria ya kimataifa, lakini zaidi ya yote, ni suala la kimaadili.”

#Chanzobbcswahili
#StarTvUpdate

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *