#HABARI: Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dennis Lazaro, amesema kuwa vita vinavyoendelea katika maeneo mbalimbali duniani vinaendelea kuathiri uzalishaji wa bidhaa, usafirishaji hali inayochangiwa na kupanda kwa bei za nishati.
Mhe. Lazaro ametoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam alipomwakilisha Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Judith Kapinga, katika mkutano wa siku mbili wa taasisi zinazoshughulikia ushindani Barani Afrika (AFC).
Amesema mkutano huo ni muhimu katika kubadilishana uzoefu na kuibua mbinu madhubuti za kumlinda mlaji, hasa katika kipindi hiki ambacho changamoto za kiuchumi zinaweza kuchochea baadhi ya wafanyabiashara kujihusisha na vitendo vya biashara haramu.
Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani (FCC), Bi. Khadija Ngasongwa, amesisitiza umuhimu wa kufanya tafiti na uchunguzi wa kina ili kuwasaidia walaji kufanya maamuzi sahihi na kulinda fedha zao katika mazingira ya sasa ya kiuchumi yanayoathiriwa na migogoro ya kimataifa, huku Mwenyekiti wa Jukwaa la Ushindani Barani Afrika (AFC), Vipin Naugah kutoka Mauritius, akiweka bayana kuwa mkutano huo una nafasi kubwa katika kuimarisha ushirikiano wa kikanda pamoja na kuweka mikakati ya pamoja ya kulinda ushindani na maslahi ya walaji.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania
(Feed generated with FetchRSS)