
Mkuu wa nchi wa Kongo, Denis Sassou-Nguesso, mwenye umri wa miaka 82, akiwa na miaka 41 madarakani, ameapishwa siku ya Alhamisi, Aprili 16, kwa muhula wake wa tano mfululizo. Alichaguliwa tena kwa asilimia 94.90 ya kura katika uchaguzi wa rais wa Machi 15. Sherehe hiyo ilifanyika katika uwanja wa Kintélé, kitongoji cha kaskazini mwa Brazzaville, mbele ya mamia ya maelfu ya Wakongo na wakuu wa nchi zaidi ya kumi kutoka Afrika, wakiwemo Paul Kagame na Félix Tshisekedi.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Na mwandishi wetu huko Brazzaville, Loïcia Martial
Kwenye jukwaa lililojengwa katikati ya uwanja, mbele ya majaji wa Mahakama ya Katiba, Rais wa Kongo Denis Sassou-Nguesso aliapa kuheshimu na kuhakikisha katiba ya Kongo-Brazzaville inaheshimiwa.
Wakati rufaa ya kiongozi wa upinzani Dave Mafoula ikikataliwa na Mahakama ya Katiba, Denis Sassou Nguesso alijitambulisha kama rais wa Wakongo wote, bila ubaguzi. “Vijana wa Wakongo, nyinyi ndio mustakabali wa Kongo. Mustakabali unaoundwa kwa sasa. Kinachofanyika leo kinatarajia majukumu na wasiwasi mtakayokabiliana nayo kesho, hivyo basi kuna hitaji la kuijua nchi, kuipenda, na kujua historia yake ,” alitangaza.
Mkuu wa nchi wa Kongo aliwataka vijana kufanya kazi kwa bidii na kuwa wanyenyekevu. Alichaguliwa kwa programu yake, “Tuendelee na kupiga hatua kuelekea maendeleo.”
Alipongezwa na marais wengine kumi wa Afrika waliokuja kuhudhuria sherehe yake ya kuapishwa, wakiwemo marais wa Angola, DRC, Rwanda, na Burundi.