Beijing imeishutumu Tokyo kwa kushindwa kuwalinda ipasavyo wanadiplomasia wa China baada ya kupokea vitisho vitatu katika kipindi cha mwezi mmoja, huku kukiwa na mvutano unaoendelea kati ya majirani hao wawili wa Asia. 

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Ubalozi wa China umeisihi Japan “kuwaadhibu vikali wahusika,” Ukielezea matukio siku ya Alhamisi kwenye mtandao wa kijamii wa X, ikiwa ni pamoja na uvamizi na tishio la bomu. 

Mnamo Machi 24, mwanamume aliyetambuliwa kama mwanachama wa Kikosi cha Kujilinda cha Japani (JSF) aliingia katika jengo la ubalozi wa China huko Tokyo na kutishia kuwaua wanadiplomasia. 

Tukio hilo lilitokea, kulingana na ubalozi, wiki chache tu baada ya kupokea barua ya vitisho kutoka kwa “kitengo cha wasomi” kinachodaiwa kuundwa na wanachama wa zamani wa JSF na polisi, ambacho kilitishia kuwaua raia wa China, shirika la habari la AFP linaripoti.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *