Waziri wa mambo ya nje wa Iran, Abbas Araghchi, amesema kuwa mlango Bahari wa Hormuz, njia kuu ya biashara ya dunia, utabakia wazi mradi tu usitishaji wa mapigano kwenye eneo la mashariki ya kati utadumu, tangazo lililopkelewa vizuri na Washington.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Punde baada ya tangazo la Waziri Abbas kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa X, rais wa Marekani Donald Trump, alilipokea kwa mikono miwili lakini akasisitiza kuwa jeshi lake litaendelea kuzuia meli zinaoingia na kutoka kwenye bandari za Iran hadi pale mkataba wa amani utakapopatikana.
Tangazo la Iran linakuja wakati huu hivi leo viongozi wa Ufaransa, Uingereza na Ujerumani wakifanya mkutano na nchi washirika kutafuta namna bora ya kuhakikisha eneo la baharí la Hormuz linakuwa wazi kwa biashara za kimataifa.
Tangu Iran itangaze kudhibiti eneo hilo la baharí, ugavi wa mafuta na gesi duniani umeshuka kwa kiwango kikubwa hali iliyotatiza upatanikajai wa nishati hiyo kwa mataifa yaliyokuwa yanategemea mafuta yao kupita kwenye njia hiyo.
Wakati huu Marekani na Iran zikiwa zimekubaliana kusitisha vita kwa wiki mbili kuanzia jula lililopita, kumeleta ahueni kwa Dunia ambayo sasa inaamini ikiwa meli zakutosha zitaruhusiwa kupita na shehena ya mafuta yliyokuwa yamekwamba kwa zaidi ya mwezi mmoja upatanikanaji wa nishati hiyo utapunguza mfumuko wa bei ambao umeanza kushika kasi kwenye mataifa mengi.