Mbunge wa Tunduru, Ado Shaibu, ameibua hoja bungeni akiitaka Serikali kutoa majibu ya kina kuhusu watu wanaodaiwa kupotea au kutekwa katika nyakati tofauti nchini.

Akichangia mjadala huo, Shaibu ametaja baadhi ya majina yaliyojitokeza katika ripoti mbalimbali, akiwamo Balozi Humphrey Polepole na ndugu yake Mlai.

Aidha, Shaibu amesisitiza kuwa ni muhimu kwa Serikali kueleza hatima ya watu wote waliotajwa pamoja na kuhakikisha kunakuwa na uchunguzi huru na wa kina.

Ameongeza kuwa kutokana na wingi wa matukio hayo, kuna haja ya kuwapo kwa uwazi zaidi ili kuondoa hofu kwa wananchi na kulinda haki za binadamu.

Akijibu hoja hiyo, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi alieleza kuwa baadhi ya kesi zimefikishwa katika vyombo vya sheria na nyingine ziko katika hatua za upelelezi, huku akibainisha kuwa zipo pia taarifa zilizodai watu kutekwa ambazo baadaye zilithibitika kuwa si za kweli.

Amesisitiza kuwa kutokana na taratibu za kisheria, masuala yaliyoko mahakamani hayawezi kujadiliwa kwa kina hadharani, huku akiongeza kuwa uchunguzi wa baadhi ya tuhuma unaendelea kwa kushirikiana na vyombo vya ndani na vya kimataifa.

#StarTvUpdate

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *